DROGBA AGOMA KUCHEZA, KISA KUPIGWA BENCHI

Mambo mchanganyiko kuhusu soka la kimataifa
offside
Posts: 6
Joined: Sat Aug 27, 2016 6:27 pm

DROGBA AGOMA KUCHEZA, KISA KUPIGWA BENCHI

Postby offside » Wed Oct 19, 2016 9:10 am

Mchezaji wa timu ya Montreal Impact inayoshiriki ligi kuu ya Marekani(MLS) Didier Drogba amegoma kucheza kabisa baada ya kocha wa timu hiyo kumuweka benchi, timu hiyo ilipocheza na timu ya Toronto. Drogba hakuonekana kabisa uwanjani hapo huku akichukizwa kabisa na kitendo cha kocha wake Mauro Biello kusingizia maumivu ya mgongo aliyokuwa nayo kuwa ndio chanzo cha yeye kuwekwa benchi. Hata hivyo uongozi wa timu hiyo umesema utakaa ili kusuluhisha tatizo hilo.
Image

Return to “Mambo Mchanganyiko”