ROONEY KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA 2018

Mada mchanganyiko kuhusu soka la Ulaya
tega
Posts: 3
Joined: Sat Aug 27, 2016 6:38 pm

ROONEY KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA 2018

Postby tega » Tue Aug 30, 2016 4:46 pm

Kwenye mkutano na waandishi wa habari leo (30 Agosti 2016), Rooney amebainisha kwamba atastaafu kuitumikia timu ya taifa ifikapo 2018, baada tu ya kombe la dunia huko Urusi. Rooney ambaye ameifungia England mabao 53 katika mechi 115 alizoichezea timu hiyo amesema kuwa 2018 utakuwa wakati muafaka kwa yeye kuondoka. "Nilianza kucheza soka la kulipwa nikiwa na miaka 16, nikiwa na miaka 17 nikaanza kuichezea timu yangu ya taifa. Miaka 15 ni mingi sana. Ntakuwa nimefikisha umri wa miaka 34 ifikapo 2018." alisema Rooney.
Kweli Rooney ni wakati wa kufikiria kuondoka, kwa sababu watu wameshaanza kukuchoka.

Return to “Soka la Ulaya”