MKWASA VIPI MBONA UNAONDOKA KWELI

Hoja, maoni, habari na ujumbe kuhusu timu yetu ya Taifa.
hbwasport
Posts: 7
Joined: Sat Aug 27, 2016 6:36 pm

MKWASA VIPI MBONA UNAONDOKA KWELI

Postby hbwasport » Wed Sep 07, 2016 10:12 am

Kocha mkuu wa Taifa Stars hana mpango wa kuendelea kukinoa kikosi cha Taifa Stars baada ya mkataba wake kuisha. Mkataba wake utaisha mwezi Machi mwakani (2017). Mkwasa amebainisha kuwa timu ya Taifa ina matatizo mengi hivyo hataendelea kuinoa timu hiyo baada ya mkataba kuisha. Matatizo aliyoyataja ni pamoja na kukosa muda wa kutosha wa kuweka kambi ili wachezaji wazoeane na kujiweka fit, wachezaji kutokuwa najezi za kubadili wakati wa mapumziko. Hapo mkwasa hujaeleweka kabisa. Hebu jaribu kutaja matatizo mengine, mi kwa upande wangu sijamuelewa

Return to “Taifa Stars”