GUARDIOLA:TOURE HATACHEZA MPAKA WAKALA AOMBE MSAMAHA

Mashabiki wa Manchester City kutoa mada mbalimbali kuhusu timu yao
offside
Posts: 6
Joined: Sat Aug 27, 2016 6:27 pm

GUARDIOLA:TOURE HATACHEZA MPAKA WAKALA AOMBE MSAMAHA

Postby offside » Wed Sep 21, 2016 9:23 am

Kocha mkuu wa Timu ya Man City ameapa kuwa kiungo wa timu hiyo hatacheza mpaka pale wakala wake Dimitri Seluk atakapoomba msamaha. Pep anamtuhumu wakala huyo kwa maneno yake ya kichochezi, pale aliposema kuwa ati Guardiola anamnyanyasa mchezaji huyo. Wakala huyo inasemekana alitoa kauli hiyo baada ya kocha Guardiola kutomuweka Yaya kwenye kikosi kilichocheza ligi ya mabingwa ulaya. Kocha huyo ameweka msimamo huo kwamba iwapo hataombwa msamaha, Yaya hatacheza mpaka mkataba wake utakapoisha mwisho wa msimu huu, na atakuwa huru kuondoka. Kumbe matatizo yako hapo!!!
Image

Return to “Manchester City Fans”